REAL MADRID YALAZIMISHA SARE NA ATHLETICO BILBAO NYUMBANI BERNABEU.


Siku moja baada ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona kuruhusu kupoteza point mbili ugenini katika mchezo wao wa Ligi Kuu Hispania LaLiga dhidi ya Celta Vigo, usiku wa April 18 wapinzani wao Real Madrid wamekutana na ugumu kama waliokutana nao wapinzania wao Barcelona kwa Celta Vigo.


Real Madrid leo wakiwakaribisha Athletic Bilbao kucheza mchezo wao wa 33 wa LaLiga katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu, Real Madrid wamelazimishwa sare ya kufungana goli 1-1, Athletic Bao lilifungwa mapema tu dakika ya 14 ya mchezo kupitia kwa Inak Williams.


Baada ya kuruhusu goli la mapema Real Madrid walilazimika kupambana hadi dakika ya 87 ndio wakapata goli la kusawazisha kupitia kwa staa wao Cristiano Ronaldo, hivyo baada ya sare hiyo Real Madrid wanaendelea kuzidiwa na wapinzania wao FC Barcelona wanaoongoza Ligi kwa tofauti ya point 15, Real Madrid wao wakibaki na michezo mitano.


Mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu