WANAMICHEZO WA TANZANIA WATOWEKA AUSTRALIA

April 17, 2018

 

 

 

 

Moja kati ya habari ambazo nimekutana nazo leo April 17 ni pamoja na hii ya mtanzania Fathiya Pazi  ambaye ni mchezaji wa mchezo wa table tennis aliyekuwa anaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Jumuiya ya Madola Goldcoast Australiakuwa ametoweka kambini.

 

 

Fathiya Pazi sio mwanamichezo pekee wa Afrika aliyetoweka katika kambi ya timu yake, pia imeripotiwa kuwa bondia Ben Agina raia wa Kenya nae ameripotiwa kutoweka wakati wa timu yake ikibadilisha ndege.

 

Hata hivyo kutoweka kwa wanamichezo hao kunadaiwa kuwa ni kutokana na wanamichezo wa afrika kupenda kuzamia ulaya kwa madai ya kwenda kutafuta maisha bora.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon