RAISI WA UFARANSA AMUOMBA TRUMP ABAKIZE MAJESHI YAKE SYRIARais wa Ufaransa, Emmanuel Macron,amesema amemshamwishi Rais wa Marekani Donald Trump, asiviondoe vikosi vya askari wa Marekani vilivyoko nchini Syria.

Mapema mwezi huu, Rais Trump alisema kwamba ataviondoa vikosi vya askari wake vipatavyo elfu mbili ambavyo vilitumwa nchini Syria hivi karibuni.

Ingawa Rais wa Macron amewaambia waandishi habari nchini mwake kwamba amezungumza na rais Trump kabla ya shambukizi la anga lililotekelezwa mwisho mwa juma lililopita na kumtaka ashiriki kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa muda mrefu zaidi.


Akitolea ufafanuzi juu ya shambulio hilo la anga lililotekelezwa kwa pamoja baina ya Marekani, Ufaransa na Uingereza kwamba lilikuwa la halali.

Na kuongeza kuwa wanawajibika kutokana na shambulizi la kemikali lililotekelezwa na Syria na kwamba hatua hiyo isichukuliwe kuwa ni tamko la vita dhidi ya Syria.

Mji wa Washington unajiandaa kuweka sheria kali zaidi kwa kwa kampuni za Urusi zenye uhusiano wa karibu na rais wa Syria, Bashar al Assad.Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, amesema kwamba hatua hizo mpya kwa serikali ya Syria inayotuhumiwa kuhusika na shambulizi la kemikali kwa raia litawekwa bayana leo Jumatatu.


Pia Nikki alikanusha ripoti kwamba Rais Trump anampango wa kuviondoa vikosi vya askari wake kutoka Siria ndani ya miezi sita. Nikki pia ameongeza kusema kuwa Washington ilikuwa na nia ya kuhakikisha hakuna matumizi zaidi ya silaha za kemikali huko Syria , na matokeo ya makombora hayo ni kukamilisha kushindwa kwa Kikundi cha Kiislamu cha Kiislamu na kudhoofisha kuenea kwa ushawishi wa Iran katika kanda.

Naye Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa upande wake amezungumzia mashambulizi hayo ya anga kwa kusema kuwa mashambulizi zaid ya anga dhidi ya Syria yanayotekelezwa na mamlaka ya Magharibi yanaweza kusababisha machafuko ya kimataifa.


Akizungumza kwa njia ya simu na rais mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, washirika wawili muhimu wa serikali ya Syria walikubali kuwa shambulio hilo la naga limeharibu nafasi ya azimio la kisiasa nchini Syria.
Nchini Syria kwenyewe, wakaguzi wa silaha za kemikali kutoka Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali wanatarajiwa kusafiri hadi eneo la mashambulizi ya gesi ya sumu huko Douma.


CHANZO:BBC


Mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu