CR 7 JUNIOR AWEKA REKODI YA UFUNGAJI SHULENI


Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Club ya Real Madrid ya HispaniaCristiano Ronaldo sasa ni wazi kuwa amepata mrithi sahihi katika kazi yake ya sokaCristiano Ronaldo Junior, Ronaldo JR ameanza kuchukua headlines akiwa bado ana umri wa miaka 7.


Kama hufahamu Cristiano Ronaldo Junior ni mtoto wa kwanza wa Cristiano Ronaldo ana umri wa miaka 7 na sasa ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kushinda tuzo mbalimbali akiwa bado ana umri wa miaka saba.

Ronaldo Junior April 14 2018 akiwa na bibi yake mzaa baba Dolores Aveiro ameshinda tuzo ya kuwa mfungaji bora wa shule baada ya msimu kumalizika, hiyo ni tuzo ya kwanza ya Ronaldo Junior kupata katika soka na Ronaldo na mama yake wote wamepost katika account zao za instagram kumpongeza Ronaldo Junior.


Kwa upande wa baba mtu mwenyewe Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi 5 kubwa Ulaya (391), UEFA Champions League (120), UEFA European Championship (29) na FIFA Club World Cup (7) na ndio mchezaji aliyefunga magoli mengi UEFA Champions League katika msimu mmoja (17).mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu