MWANASIASA MKONGWE KENYA AFARIKI DUNIA

April 16, 2018

 

 

 

Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Matiba, aliaga dunia hapo jana akiwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen, ijini Nairobi.

Matiba ambaye ni maarufu katika siasa za ukombozi wa pili wa kisiasa nchini Kenya, baada ya ile ya Uhuru miaka ya 1950s na 1960s.

 

Mwanasiasa huyo maarufu ambaye alitatiza pakubwa siasa za Rais wa awamu ya pili nchini Kenya
alzaliwa katika Wilaya Muranga, iliyoko maeneo ya katikati mwa Kenya.

Alikuwa mwanasiasa ambaye daima alikuwa akitabasamu, na mkereketwa wa kutetea haki za kibinadamu na kuwepo kwa demokrasia nchini Kenya.

Aliwania kiti cha urais mwaka wa 1992, lakini akaibuka wa pili, nyuma ya Daniel Toroitich Arap Moi.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon