Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

MSHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA YAMALIZIKA HUKU TANZANIA TUKIAMBULIA PATUPU

April 16, 2018

 

 

 

 

Mashindano ya Commonwealth yamemalizika jana Australia yakiwa ni mashindano ya 21 yakishirikisha mataifa 71 yaliyowahi kutawaliwa na Uingeteza yakianza tarehe 4 April mpaka 15 April mwaka huu.

Wenyeji Australia ndiyo taifa lililopeleka wanamichezo wengi zaidi likipeleka watu 474 na Gambia wakipeleka watu wachache zaidi ikiwa ni wanamichezo 6 pekee.

Takribani medali 1500 zimetolewa na Tanzania hatujarudisha nyumbani hata moja, Australia wakibakisha nyumbani medali 198, Afrika Kusini wakitubeba Afrika kwa kubeba medali 37 na Nigeria wakiondoka na medali 24.

Kwa Afrika Mashariki Kenya wametutoa kimasomaso wakichukua medali 17 ( dhahabu 4, fedha 7, shaba 6), Uganda wamebeba shani 6 (3 za dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba). Tanzania na Rwanda tulienda kama washiriki kwani tumerudi mikono mitupu.

Sababu ya Kenya na Uganda kurudi na medali inaweza ikawa imechagizwa na kupeleka kikosi kikubwa cha wanamichezo, Kenya ikipeleka 138, Uganda 70, Tanzania 19 na Rwanda 17

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload