Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

AFUNGWA JELA BAADA YA KUHAMASISHA MUUNGANO

April 16, 2018

 

 

 

 

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuhamasisha Somaliland kuungana na Somalia .

Makundi ya wanaharakati nchini Somaliland wamesema Bi. Nacima Qorane ameminywa haki zake za kibinadamu.

 

Somaliland ilijitambulisha kuwa huru mwaka 1991 licha ya kuwa taifa hilo halitambuliwi kimataifa.

Bi.Qorane alikamatwa mwezi Januari baada ya kurejea kutoka Mogadishu,mji mkuu wa Somalia ,wakati ambapo mshtakiwa alisema ametoka kuimba shairi la kuhamasisha umoja wa Somalia.

Baada ya mapigano ya mara kwa mara kaskazini magharibi mwa Somalia,hali hiyo ilisababisha mgawanyiko wa nchi hiyo na hatimaye Somaliland ikajitangaza kuwa iko huru 

 

Eneo hilo la Somaliland lina wakazi wapatao milioni 3.5

Mwendesha mashtaka amesema msichana huyo amepatikana na makosa ya kuitukana nchi yake na kutokuwa mzalendo wa serikali yake ya Somaliland.

Kituo cha haki za binadamu nchini Somaliland ameiomba serikali ya Somaliland kumuachia huru Nacima Qorane na kuheshimu haki za binadamu.

 

"Uhuru wa kujieleza ni jambo ambalo linalindwa na katiba ya Somaliland.Hivyo tumeitaka Somaliland kuheshimu katika yake yenyewe."

Mkurugenzi wa kituo hicho Guleid Ahmed Jama aliiambia BBC juu ya hofu yao kwa kukamatwa na kufungwa kwa msichana yule.

 

Aidha yeye sio wa kwanza kukutana na mashtaka ya namna hii kwa kuwa kuna idadi kubwa ya waandishi wa habari na wasanii waliowahi kufungwa Somaliland kwa kosa la namna hiyo hiyo.

 

CHANZO:BBC

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload