Untitled

Michezo ya Jumuiya ya Madola inamalizika wikendi hii mjini Gold Coast, Australia huku wenyeji bado wakiwa kileleni.

Mpaka sasa Australia inaongoza na dhahabu 63, fedha 48 na shaba 50 ikifuatiwa na England, India, Canada na Afrika Kusini katika nafasi ya tano.

Afrika Kusini ndilo taifa linaloongoza washiriki wa Afrika na dhahabu 11, fedha 10 na shaba 12. Nigeria wako katika nafasi ya 12, Botswana 15, Uganda 17, Kenya 18, Mauritius 28, Cameroon na Ghana wote katika nafasi ya 33.

Kuna kivumbi Ijumaa hii hasa katika riadha na mchezo wa raga kwa wanaume na wanawake.

Image captionTimu ya raga ya Uganda iko uwanjani wikendi hii

Hii ni mara ya kwanza raga ya wanawake inafanyika katika michezo hii.

Bingwa wa Olimpiki Australia wako kundi B pamoja na Fiji, England na Wales. Kundi B kuna New Zealand, Canada, Afrika Kusini na Kenya.

Kenya, Zambia, Canada na New Zealand wako kundi C huku Uganda wakiwa kundi D na Fiji, Wales na Sri Lanka.Hii ni mara ya sita raga ya wanaume inafanyika katika michezo ya Jumuiya ya Madola, mara ya kwanza ikiwa ni 1998 huko Kuala Lumpur, Malaysia, mshindi akawa ni New Zealand ambayo ilishikilia kombe hilo mpaka michezo ya 2014 Afrika Kusini ilipoibuka mshindi.

Ulingoni wa ndondi, mabondia wa Kenya na Uganda Ijumaa wiki hii wamepoteza mapigano yao ya nusu-fainali.


Christine Ongare wa Kenya ameshindwa na Carly McNaul wa Ireland ya Kaskazini kwa pointi uzani wa fly. Hatahivyo atarudi nyumbani na shaba.

Nimefurahishwa na matokeo yangu lakini nahimiza serikali itilie maanani ndondi za wanawake, nataka sana nipate kazi ndio wanawake wenzangu wajue faida ya mchezo

Christine Ongare, Bondia wa Kenya

``Nimefurahishwa na matokeo yangu lakini nahimiza serikali itilie maanani ndondi za wanawake, nataka sana nipate kazi ndio wanawake wenzangu wajue faida ya mchezo,'' anasema Ongare.


Bondia wa Uganda Juma Miiro naye pia amepata shaba baada ya kushindwa kwa pointi na Amit wa India uzani wa light-fly.

Miiro anasema sasa anataka kujiunga na ndondi za kulipqwa nchini Australia.

Kuna ngoma kwenye riadha kwani Ijumaa wiki hii ni fainali ya mbio za mita elfu kumi, mita elfu tatu kuruka vizuizi na maji na mita mia nane za wanawake.

Bingwa wa Olimpiki Caster Semenya atapambana vikali na waakilishi wa Kenya Margaret Nyairera, Eglay Nalianya na Emily Cherotich. Kutoka Uganda ni Dorcus Ajok na Winnie Nanyondo.


Je, Kenya itaendelea kutawala mbio za mita elfu tatu kuruka vizuizi na maji? Hilo ndilo swali wataalam wa riadha wanajiuliza.

Bingwa wa Olimpiki Conseslus Kipruto anatarajiwa kushinda dhahabu.

Kutakua na ushindani mkali kati ya wanariadha wa Kenya na Uganda mbio za mita elfu kumi.

Joshua Cheptegei wa Uganda ananuia kupata dhahabu ya pili baada ya kuangusha wanariadha wa Kenya mbio za mita elfu tano.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu