ALIYOYASEMA MAKONDA KUHUSU ZOEZI LA KUWASAIDIA WALIOKIMBIWA


Leo April 14, 2018 Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ameongea LIVE katika vituo vya television nchini kuhusiana na zoezi la kuwasaidia wakina Mama waliotelekezewa watoto na Waume zao, Mzunguko.com tunakusogezea Mambo 8 aliyoyazungumza RC siku ya leo.


“Makonda anaelekea wapi, mbona kila kitu akikifanya kinakuwa kikubwa, utagombana na MUNGU bure, sababu mawazo mengine ukitaka kufanikiwa ndugu yangu na Wanasiasa wenzangu, ombi langu na ushauri wangu wekeni ibada zenu sawa kwa MUNGU wenu, ukitaka kufanya mambo makubwa mtangulize MUNGU kama Rais Magufuli anavyosema” -RC Makonda


“MUNGU akikaa ndani yako atafungua milango, piga mahesabu kuna Bima watoto wanapata matibabu bure manake watoto watakaokanyaga pale watalipiwa na hapo kuna mtu mmoja kaona, kasema nikusaidie nini?,” -RC Makonda


“nikamwambia Mimi shauku yangu angalau wakati Serikali inashughulikia haki ya mtoto , basi apate matibabu angalau kwa mwaka mmoja, tena sio Mtanzania, sisi Watanzania tumebaki tunaangaika kutafuta mapungufu” -RC Makonda


“Msouth Afrika katoa mwaka mmoja wewe Mtanzania ambaye jirani yako ndio anaangaika wajibu wako ni nini? swali hili liende kwa kila mtu, jukumu la kwanza la Serikali sio kumkatia Bima, jukumu la kwanza la Serikali ni wajibu wa Baba na Mama kumtunza mtoto, sheria inasema kutomtunza mtoto kwa pande zote mbili ni kosa la jinai” -RC Makonda


“Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, lakini ndo msimamizi wa shughuli zote za Serikali katika mkoa, mtu yoyote anaekaidi wito wa ustawi wa jamii ambao wako chini yangu, kwa mamlaka niliyonayo nakutia ndani any time,” -RC Makonda

“Bahati mbaya kwangu sheria ina nafasi kubwa sana kuliko hadhi unayojitengenezea ambayo kimsingi huna kama umetekeleza Mtoto, tusijaribiane, usitake kupima uwezo wangu” -RC Makonda


“Kukaidi wito ni jambo lingine, kupata matokeo ya kwamba wewe ni mzazi sio mzazi ni jambo jigine, kwa hiyo unapoitwa ukikaidi unakutana na matokeo ya kukaidi kutawanyika, tunapokuita hatukuiti sababu umepima DNA, unapokataa maana yake umekataa wito halali na kama Mwananchi anaenda kwa RC anakuita hutaki maana yake umemuweka mfukoni RC” -RC Makonda


“Huchafuliwi kama una mtoto wewe ndo umejichafua kama umetoka nje ya ndo wewe ndo umejichafua, kama umeamua kuzaa nje ya utaratibu wewe ndo umejichafua, sisi hatuwezi kuja kukuchafua kwa matendo yako, matendo yako ndo yamekuchafua” -RC Makonda


MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu