SERGIO RAMOS AIKWEPA ADHABU YA KUFUNGIWA


sergio ramosBeki wa Real Madrid Sergio Ramos ameokoka na adhabu kwa kuangalia mechi ya juzi dhidi ya Juventus kwenye njia ya kuingilia na kutokea wachezaji. Awali iliaminika kuwa Ramos anaweza kufungiwa mechi ya kwanza ya nusu fainali, lakini haijawa hivyo, UEFA wamesema kuwa hakuna sababu za kutoa adhabu yoyote ya kinidhamu kwa mchezaji huyo. Imeripotiwa kuwa UEFA wameona Ramos hakuvunja sheria yoyote kutokana hakuondoka katika "Tunnel" ( kwenye njia ya kuingilia na kutokea wachezaji). . Sheria za UEFA hazizui wachezaji waliofungiwa kuwepo kwenye "Tunnel" au katika vyumba vya kubadilishia nguo.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu