BAADA YA VIDEO CHAFU KUZAGAA MSANII NANDY AOMBA RADHI
Siku ya April 12,2018 video ambayo ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii ni video ikiwaonyesha Nandy na Bill Nas wakiwa mapenzini na mashabiki kuachia comments zao juu ya video hiyo iliyowaudhi mashabiki wengi wa muziki wa bongo fleva.


Kupitia instagram account ya Nandy alionekana kuomba radhi kwa mashabiki na watu wake wote wa karibu kutokana na video hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na pia leo April 13,2018 Nandy amezidi kuomba radhi kwa kilichotokea ila kwa upande wa Bill Nas amejitetea katika ukurasa wake wa instagram kwa kusema kwamba hajui lolote kuhusu video hiyo iliyochukuliwa kwa simu.


“Kiukweli niko katika wakati mgumu wa maisha yangu.. jana sikuwa sawa ila leo nimeweza hata shika simu yangu najua matusi yote na fedhea kutoka kwa mashabiki wangu ni sababu wanaamini hili ni kusudio letu au langu hii video iwe public naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea!!! sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida”


“Sitakiwi kujieleza sana ila naamini nikiandika hili nitakaa na amani kwa ambaye ataamuaa kuendelea kunihukumu aendelee tu kunihukumu kwani kweli nimekosea ila ajiulize kama yeye hajawahi kukosea!” -Nandy


aliongeza na kusema,


“Mambo yetu wote ya private yanatakiwa kubaki private, aliyeyatoa amefanikiwa kuleta hii taharuki, sintofahamu na maumivu makubwa ambayo sijawahi kupata maishani mwangu. ila Naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!!”


Nilibadili simu yangu mara 2 toka 2016 na Bilnas aliibiiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake, so hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani? maswali ni mengi matusi ni mengi simu na sms ni nyingi mnoo… naumiaa naumiaa kupita kiasi.” -Nandy aliongeza


Nandy leo tarehe 13/4/ 2018 ameonekana kwenda BASATA ili kuweka mambo yake sawa kutokana na video yake na Bill Nas kusambaa katika mitandao ya kijamii.mzunguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu