AUSTRALIA WAKABIDHI MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA BIRMINGHAMJumapili hii mji wa Gold Coast Australia utaukabidhi kijiti cha uenyeji wa michezo ya jumuiya ya madola mji wa Birmingham wa Uingereza.Birmingham inategemea kuwa mwenyeji wa michuano ya jumuiya ya madola ya mwaka 2022.


Mpango wa paundi milioni 70 kukipanua na kukiboresha Alexander Stadium ya Birmingam umetangazwa.Mpango huo utakiboresha kiwanja hicho chenye umri wa Zaidi ya miaka 40 kutoka kuweza kubeba watu 12,700 mpaka watu 40,000.Tayari picha ya namna kiwanja hicho kinavyotarajiwa kuonekana imewekwa wazi na iwapo mpango utasalia ulivyo basi nchi nyingi zitaweza kuziona rangi za bendera zao kwani paa la Uwanja huo litakuwa na mifuniko ambayo ina rangi za bendera za nchi kadhaa Duniani.


Image captionuwanja huu una umri wa zaidi ya miaka 40, hivi ndivyo unavyoonekana kwa nje

Upanuzi huu utakifanya pia kiwanja hiki kuwa kikubwa zaidi chenye uwezo wa kutumika kwa michezo mbalimbali ya riadha, ukiacha vile vilivyoko London.


Munguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu