Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

SIMBA WAIBUKA NA USHINDI MNONO DHIDI YA MBEYA CITY

April 12, 2018

 

 

 

 

 

Club ya wekundu wa Msimbazi Simba SC leo April 12 2018 ilicheza mchezo wake wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya club ya Mbeya City ya Mbeya uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

 

Simba wanacheza game hiyo ikiwa ni siku moja imepita toka watani zao wa jadi Yanga wapoteze point 2 dhidi ya Singida baada ya kutoka sare ya 1-1, Simba leo wamecheza game yao bila presha baada ya jana Yanga kutengeneza gap la point 5 nyuma ya Simba.

 

Hivyo leo Simba wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mbeya City, magoli ya Simba yakifungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 17, Asante Kwasi dakika ya 32 na John Bocco dakika ya 35, ushindi huo umemfanya Simba aendelee kuongoza Ligi kwa tofauti ya point 8 dhidi  ya Yanga wanaofuatia kwa kuwa na point 47 ila Simba kaizidi Yanga mchezo mmoja.

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload