Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

PENALTI YA UTATA YAIVUSHA REAL MADRID NUSU FAINALI UEFA

April 12, 2018

 

 

 

Usiku wa April 10 na usiku wa April 11 2018 ilichezwa michezo ya marudiano ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, inawezekana michezo hiyo ndio imekuwa na mvuto zaidi ya michezo yote ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwa miaka ya hivi karibuni.

 

 

 

 

Baada ya AS Roma kuushangaza ulimwengu kwa kuitoa FC Barcelona ya Hispania kwa aggregate ya 4-4, licha ya kuwa walianza kwa kuwa nyuma kwa magoli 4-1 yaliofungwa mchezo wa kwanza, Juventus nao leo almanusura waushangaze ulimwengu katika mchezo wao  dhidi ya Real Madrid.

 

Juventus walifanikiwa na wao kufunga magoli 3-0 katika mchezo wa marudiano kama ilivyokuwa kwa Real Madrid mchezo wa kwanza ila dakika za nyongeza zikawa chungu kwa Juventus baada ya muamuzi Michale Oliver kutoa penalti kwa Real Madrid dakika za nyongeza baada ya Medhi Benatia kumchezea faulo Lucas Vazquez katika eneo la hatari.

Tukio lililopelekea refa Michael Oliver kutoa mkwaju huo wa hatari.

 

 

 

 

 

 

 

Baada ya maamuzi ya refa Michael Oliver kutoa penalti ndipo Cristiano Ronaldo alipopiga na kuifungia Real Madrid goli na kuufanya mchezo kumalizika kwa Juventus  kupata ushindi wa magoli 3-1 lakini wametolewa katika michuano hiyo kwa aggregate ya jumla ya magoli 4-3.

 

Magoli ya Juventus yalifungwa na Mario Mandzukic dakika ya 2, 37 na Blaise Matuidi  dakika ya 61, hivyo game za robo fainali zimemalizika kwa vilabu vya FC Bayern Munich,Real Madrid, Liverpool na AS Roma kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano yaChampions League.

 

 

mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload