KENYATA AKUBALI KUGAWA PEDI BURE KWA WANAFUNZI WA KIKE

April 12, 2018

 

 

 

Jana  April 11, 2018  kutoka nchini Kenya ambapo Rais Uhuru Kenyatta amesaini muswada ambao sasa utakuwa sheria kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.

 

Kenyatta amesaini sheria hiyo April 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.

Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon