AMOAH WA AZAM FC ATAKUWA NJE KWA MIEZI 9


Club ya Azam FC leo kupitia afisa habari wake Jafari Iddi Maganga imekutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa mbalimbali kuhusiana na mwenendo wa club yao kuelekea mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting na hali za majeruhi.


Jafari Iddi amethibitisha kuwa maandalizi yapo sawa na kuelekea mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting April 12 2018 katika uwanja wa Mabatini ila kwa upande wa majeruhi ni kuwa Mwantika yupo nyumbani akiendelea kufanyiwa uchunguzi.


Kwa upande wa Amoah yeye baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini amesharejea nchini atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9 akiuguza jeraha lake la goti alilofanyiwa upasuaji na ugoko.


Mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu