CHANJO MPYA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI YAZINDULIWA

April 11, 2018

 

 

 

 

 

 

Serikali imezindua kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.

Zaidi ya wasichana laki 6 walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14 watachanjwa nchini nzima.

Huenda chanjo hii ikawakomboa wanawake na wasichana wengi kama wakijitokeza na kupata chanjo mapema zaidi.

 

"Saratani ya shingo ya kizazi ndio inayojitokeza zaidi Tanzania na ni chanzo cha vifo na magonjwa yanayohusiana na saratani miongoni mwa wanawake nchini."meneja wa mradi Daphrosa Lyimo  Alisema.

 

"Duniani, kuna zaidi ya wanawake 260,000 wanaofariki kwa sababu ya saratani hii, ambayo inazuilika na inatibiwa ikigunduliwa mapema." aliongezea Bwana Lyimo

Serikali ina matumaini kuwa kampeni hiyo itapunguza gharama za afya. Kumuuguza mgonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kunaweza kugharimu takriban dola za Marekani elfu 2 wakati dola 15 zitatumika kuwachanja wasichana maafisa walisema.

Mambo kumi unayoweza kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:

 • Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote

 • Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi

 • Kula chakula chenye afya

 • Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani

 • Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV

 • Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.

 • Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba

 • Jishughulishe kuupa mwili mazoezi

 • Punguza unywaji wa pombe

 • Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo                                                    

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
 • YouTube Social Icon
 • Twitter Social Icon
 • Black Instagram Icon
 • Facebook Social Icon