JE MAN CITY WATAFANYA MAAJABU DHIDI YA LIVERPOOL LEO?Leo katika Uwanja wa Etihad mjini Manchester, vijana wa mji huo Manchester City wanawakaribisha vijana kutoka mjini Liverpool.

Ni katika mchezo wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya ambapo kwa hakika Man City wana kibarua kizito sana kwani wanatakiwa kuifunga Liverpool bao 4-0 maana mechi iliyopita, Man City walibamizwa 3-0 pale Anfield mjini Liverpool.


Kiungo wa City, Fernandinho mwenye umri wa miaka 32 anasema lile juma gumu lililowakabili la kuchapwa kila walikoenda sasa limeisha na ni wakati sasa wa wachezaji wazoefu kuchukua nafasi yao na kuliongoza Jahazi.

Tangu Man City walipopoteza pale Anfield jumatano, pia katika ligi walichapwa 3-2 na Manchester United.

Liverpool ilifunga mara tatu ndani ya dakika 19 za kipindi cha kwanza katika mzunguko wa kwanza.


​Ikiwa upande wa Jurgen Klopp utaweza kushinda katika Uwanja wa Etihad, City watalazimika kushinda angalau mara tano ili kuendelea kufikia nafasi ya nne.

Ni Timu mbili pekee katika historia ya Champions League ambazo zimewahi kujikwamua kutoka katika deni la magoli matatu au Zaidi katika kipindi cha mtoano. Sawa na deni analokabiliana nalo Man City.Deportivo La Coruna ikiwa nyuma ya AC Milan 4-1 mwaka 2004 walifanikiwa kupindua matokeo kwa 4-0 in katika mechi ya marudiano.

Katika siku za hivi karibuni, ni Barcelona iliyobadilisha matokeo ya 4-0 dhidi ya Paris St-Germain kwa kushinda 6-1 katika mechi ya marudio uwanja wa Noe Camp msimu uliopita.


Katika mchezo mwingine wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya, Roma itashuhudiwa wakikwaana na Barcelona katika uwanja wa Stadio Olimpico.

Meneja wa Roma Eusebio di Francesco amekiri kwamba kwa hakika kukutana na Barcelona anakutana na alichokiita Mashine lakini anabaki na matumaini makubwa.

Waitaliano hao wanakutana na Wahispania huku waitaliano wakiwa na hasira za kuchapwa bao 4-1 katika mzunguko wa kwanza.


Pia Roma walichapwa 2-0 na Fiorentina aliyeko nafasi ya saba na sasa wana point 21 nyuma ya viongozi wa Seria A Juventus

Katika hali ya tofauti, Barcelona wakiwa na Lionell Messi wako pointi 11 juu na bado Meneja wao Ernesto Valverde pamoja na kuwa watakuja na faida ya magoli matatu kibindoni bado amesema mechi hii dhidi ya Roma hawataichukulia kawaida na kwa hakika wataingia Uwanjani kama vile matokeo ni 0-0.MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu