Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

TRUMP AKANA MALIPO YA BI DANIELS

April 6, 2018

 

 

 

 

 

Rais Trump amesema kuwa hakufahamu kuhusu malipo ya fedha za Kimarekani 130,000 yaliyolipwa na wakili wakili kwa mchezaji filamu za utupu Stormy Daniel kabla ya uchaguzi wa 2016.

 

Hii ni mara yake ya kwanza kuzungumzia swala hilo.

Alipoulizwa alipokuwa kwenye ndege ya Air Force One kama alifahamu kuhusu malipo hao na hela zilipotoka , Bwana Trump alisema "Hapana"

Alipoulizwa kwa nini wakili wake Michael Cohen alifanya malipo hayo, Bwana Trump alisema: "Inabidi umuulize Michael"

Muigizaji huyo anasema alifanya tendo la ndoa na Bwana Trump mwaka 2006. Bwana Trump amekana madai hayo.

 

Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford,anasema alisaini makubaliano ya kubaki kimya kuhusu mashusiano yake na Bw Trump na kulipwa dola za Marekani 130,000 mwezi Oktoba 2016, kabla ya uchaguzi wa urais.

 

Bi Daniels, ameiambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa alitishiwa mwaka 2017  na mtu ambaye hakumfahamu aliye wambia "kumwacha Trump"

Mawakili wa Bw Trump wanataka kulipwa fidia ya $20m (£14m) na mwanamke huyo, wakisema alikiuka makubaliano ya kuweka siri ambayo aliyatia saini katika ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

 

Mzunguko.com

 

 

 

Mwanamke huyo anasema madai hayo hayana msingi

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload