CONOR MCGREGOR AJISALIMISHA POLISI

April 6, 2018


 

 

 

Mpiganaji wa Lightweight division UFC Connor Mcgregor amejisalimisha kwa vyombo vya usalama baada ya kulishambulia basi lililobeba wapiganaji wa UFC.

Jana ilikuwa ni siku ya ku-promote event ya UFC ambayo ni UFC 223 inayopigwa kesho ambapo basi hilo lilibeba wote watakaopambana kesho wakiwamo watakaocheza pambano kuu Khabib Nurmagomedov na Max Holloway ukiwa ni mpambano wa kuamua mkanda wa Lightweight anauchukua nani.

Mcgregor alitokea kusikojulikana na kurusha kingazi kidogo cha chuma na kukirusha kwenye gari hiyo na kupasua kioo kitendo kilichofanya baadhi ya mapambano kughairishwa kesho baada ya glasi zilizovunjika kuwadhuru baadhi ya wapiganaji waliopo ndani.

Mapambano yaliyoghairishwa ni pamoja na la Chiesa aliyeumia vs Anthony Pettis, Ray Borg aliyeumia vs Brandon Moreno na lingine la Artem Lobov ambaye ametolewa kutokana na uhusika wake.

Connor bado alionekana anachukua viti na kuvirusha kwa hasira kubwa lakini waliokuwa naye walitumia nguvu kumdhibiti asisababishe madhara zaidi, tukio hilo lilitokea Barclays Centre ambapo wapiganaji walitoka kukutana na waandishi wa habari.

Mkanda wa Lightweight ulikuwa unashikiliwa na Mcgregor mpaka jana ambapo alinyang'anywa baada ya kushindwa kuutetea tangu aupate November 2016 ikiwa ni moja ya sababu inayosemwa kupelekea Connor kufanya fujo.

Sababu nyingine inayosemwa ni kwa kile kilichoripotiwa kwamba camp ya Khabib (anayegombania mkanda wa lightweight kesho) kutaka kumpiga rafiki wa karibu na training partner wake Artem Lobov siku mbili zilizopita na Mcgregor na timu yake walitoka Dublin kuja kulipiza kisasi.

Kwa sasa Connor amejisalimisha na yupo chini ya New York Police Department akishtakiwa kwa mashtaka matatu ya ushambulizi na moja la kihalifu.

Raisi wa UFC Dana White amesema anatarajia wote waliopata madhila kumfungulia mashtaka

 

Connor na kwa suala la kumtimua hawezi kumfukuza kwani Mcgregor ni mpiganaji anayejitegemea

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon