Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

MTOTO WA MOURINHO AONEKANA BENCHI LA UFUNDI LA MANCHESTER UNITED

April 5, 2018

 

Mtoto wa kocha mkuu wa Man United Jose Mourinho, Jose Junior (anafahamika kwa jina la Zuca na familia yake) mwenye umri wa miaka 17 ameonekana akiwa kwenye benchi la ufundi kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Swansea juzi jumamosi.

Kupitia kurasa ya Twitter ya Kiungo wa zamani Michael Carrick ambaye bado hajajiunga rasmi na benchi la ufundi ikiwa bado anajifunza mawili matatu akipata uzoefu, alipost picha Twitter iliyomwonesha yeye, Mourinho na mtoto Mourinho pamoja na wasaidizi wengine.

 

Mwaka jana Mourinho kupitia chaneli ya TV huko nchini Ureno alisema kijana wake huyo amekuwa akimfuata na kumshauri mambo mbalimbali kuhusu United hasahasa pale United ikifanya vibaya, akitolea mfano walivyofungwa na Watford na Man City September 2016 Jose jr aliandaa takwimu za United na kutokana na zilivyokuwa nzuri Mou aliwapelekea benchi lake na kuwaambia kimasihara wasaidizi wake kwamba mtoto wake atakuja kurithi nafasi ya mmoja wao siku moja.

 

Jose jr alijiunga na Fulham 2016 kama mlinda mlango lakini mkataba kati ya timu hiyo na yeye ulivunjwa Machi mwaka jana baada ya kufikia makubaliano.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload