MKURUGENZI WA TIA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUJUMU UCHUMI
Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Zodo Zodo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Shilingi Milioni 147,256,661.53


Akimsomea hati ya mashtaka Wakili wa TAKUKURU, Max Ali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la uhujumu uchumi.

Inadaiwa kosa hilo amelitienda May 1,2014 na May 1,2016 akiwa mwajiriwa wa Taasisi ya uhasibu Tanzania na Mkurugenzi wa huduma na uwezeshaji ambapo alishindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Shilingi Milion 147,256,661.53


Baada ya kusomewa kosa hilo mshtakiwa alikana kosa na kwamba mahakama hiyo imepewa kibali na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) cha kuendea kuisikiliza kesi hiyo.

Wakili Ali amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Wakili wa utetezi Januari Jonson aliomba mahakama impatie mteja wake dhamana na kwamba mshtakiwa yuko tayari kutimiza masharti yatakayotolewa.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Simba alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo moja atatoa fedha tasilimu Sh. Milion 73,000,700 ambayo ni nusu ya hasara aliyosababisha au mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho.


Pia mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani na asitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha mahakama.

Baada ya kutoa masharti hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi April 16,2018 kwa ajili ya kutajwa.


MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu