IBRAHIMOVIC ATAMANI GOLI LA RONALDO LINGEFUNGWA UMBALI WA MITA 40

April 4, 2018

 

 

Moja kati ya stori zilizochukua headlines katika soka la Ulaya jana ni pamoja na goli la staa wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo alilolifunga katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya UEFA Champions League dhidi yaJuventus.

 

Mchezo huo ulimalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli mawili yakifungwa na staa wa timu hiyo Chistiano Ronaldo na moja la mwisho likifungwa na Marcelo ila goli la pili la Ronaldo alilofunga kwa tiki taka ndio limeacha headlines kwa mashabiki wa soka na wachezaji ambao kila mmoja kalitolea maoni yake.

 

Staa wa zamani wa Man United ambaye anaichezea LA Galaxy ya Marekani kwa sasa Zlatan Ibrahimovic ambaye amewahi kufunga goli linalotaka kufanana na goli laRonaldo ila yeye ilikuwa ni game ya Sweden dhidi ya England amelizungumzia goli hilo“Lilikuwa goli zuri lakini angejaribu kufunga vile kutokea umbali wa mita 40”

 

mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon