KWANINI VARDY AVAE VIATU VYA CR 7?

March 30, 2018

 

 

 

 

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England Jamie Vardy katika mechi ya kirafiki jumanne hii dhidi ya Italy ambapo alifunga goli katika sare ya 1-1, alionekana amevaa viatu vya Cristiano Ronaldo. 
Kwa nini alivaa viatu hivyo ?. Jamie Vardy kwa sasa hana makubaliano mazuri na kampuni yake inayomdhamini katika viatu, Nike, hivyo viatu anavyovaa uwanjani amekuwa akinunua mwenyewe.

Imeelezwa kuwa Nike walitaka kumpatia aina mpya ya viatu,lakini yeye hakuvipenda. 
Tangu Januari 31 mwaka huu Vardy akaacha kuvaa viatu vya Nike, akaanza kwenda katika maduka ya mtaani, anatoa pesa yake mfukoni na kununua viatu ya CR7 .

Tangu alipoanza kununua viatu hivyo, amefunga katika mechi 3 mfululizo, na pia kufunga mara 6 katika mechi 9.

Mkataba wake na Nike unafikia kikomo mwisho wa msimu huu, hivyo huenda akaendelea kuvaa viatu vya CR7 mpaka pale itakapoelezwa vinginevyo.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon