VITUO VYA MATANGAZO YA REDIO VYAFUNGIWA UGANDA

Tume ya mawasiliano nchini Uganda, UCC, imefunga vituo 23 vya redio vya FM.

Vituo hivyo vinashutumiwa kwa kutangaza 'uganga wa kienyeji na kuwatapeli wananchi.'

Hatua hiyo inafuata onyo la tangu zamani viache kuwaweka hewani waganga wa kienyeji.

Tangazo hilo la kufungiwa vituo vya redio 23 limetolewa jana jioni na mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano Godfrey Mutabazi.

Baadhi ya vituo hivyo 23 ni kutoka wilaya mbalimbali zikiwemo redio mbili za jiji Kampala ambazo ni Metro FM, Dembe FM inayomilikiwa na gazeti la Monitor, nyingine ni kutoka sehemu mbalimbali za nchi mashariki , kaskazini na magaharibi mwa Uganda.Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu