RAISI WA UFANSA AMUAGA ASKARI ALIYEUWA


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, hapo jana aliongoza hafla ya kitaifa ya kumuaga polisi aliyejiwasilisha kama mateka kwa niaba ya mwanamke mmoja wakati wa shambulizi lililofanywa na jamaa mwenye itikadi kali za Kiislamu na aliyekuwa na bunduki katika duka moja kuu kusini mwa Ufaransa wiki iliyopita.

Ushujaa huo wa kanali Arnaud Beltrame mwenye umri wa miaka 44 umesifiwa pakubwa.

Betrame alipigwa risasi na kuchomwa kisu na mshukiwa huyo na aliaga dunia siku moja baada ya shambulizi.

Zaidi ya watu 240 wameuawa Ufaransa katika mshambulizi yanayofanywa na watu wenye itikadi kali za Kiislamu nchini humo tangu mwaka 2015.


MZUNGUKO.COMTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu