TRUMP ATAKA KUKUTANA NA KIM

March 29, 2018

 

 

 

 

 

Rais wa Marekani Donald Trump, kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yuko tayari kukutana naye.

Rais Trump amedai kuwa alipokea ujumbe jana usiku kutoka kwa rais wa China Xi Jinping akimweleza kuwa mkutano kati yake na Kim Jong Un uliendelea vizuri na kwamba Kim anatarajia kukutana naye.

Hata hivyo Trump amesema kuwa, kwa sasa shinikizo pamoja na vikwazo vya juu vilivyowekwa dhidi ya Korea Kaskazini sharti vitekelezwe kwa vyovyote vile.

 

MZUNGUKO.COM

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon