MNANGAGWA AWALAUMU WAPINZANI

March 29, 2018

 

 

 

 

Rais Emmerson Mnangagwa amesema kwamba vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vilitoa taarifa za kupotosha kwa serikali ya Marekani na kupelekea kuongezwa kwa muda wa vikwazo dhidi ya nchi yake.

Wiki iliyopita, Marekani iliongeza muda wa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya serikali ya Zimbabwe kupinga sera zake za umiliki wa ardhi. Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Abidjan, Cote d’Ivoire, Mnangagwa alisema kwamba maseneta wa Marekani Jeff Flake na Chris Coons watajua ukweli wa mambo watakapozuru Zimbabwe hivi karibuni. “Ukiangalia wanachosema basi unagundua kwamba wamepotoshwa,” alisema Mnangagwa. Viongozi hao wa upinzani wakiongozwa na MDC walienda Marekani punde tu baada ya kuapishwa kwa Mnangagwa kutoa msukumo kwa serikali ya Marekani kuendeleza vikwazo dhidi ya nchi yao.

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon