MAHAKAMA YAAMURU SETH AKATIBIWE MUHIMBILI
Tarehe 28, machi 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa IPTL, Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospital ya Taifa Muhimbili baada ya mshtakiwa huyo kulalamika afya yake imearibika sana.


Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bilioni 309.


Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na pia wanafatilia vielelezo vya upelelezi nje ya nchi.


Baada ya kueleza hayo, Seth alisimama na kumueleza Hakimu Shaidi kuwa; Afya yangu imearibika sana, nahitaji kupelekwa hospitali.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema ni dhahiri afya ya mshtakiwa ikiangaliwa hata kwa macho inaonekana ni dhahifu.


“Naamuru mshtakiwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili afya yake iwe njema,” amesema Hakimu Shaidi na kuahirisha kesi hiyo hadi April 11,2018.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, milioni na Sh, bilion 309.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu