RAISI AWAOMBA MAASKOFU WAZUNGUMZIE NA VIWANDA

March 27, 2018

 

 

 

 

 

Wakati wa waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua mjadala mkubwa nchini Tanzania.

Rais Magufuli amewaomba wahubiri na maaskofu wazungumzie ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi.

Amesema hayo akiwa katika halfa fupi jijini Dar es salaam ya ugawaji wa magari ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka uliosomwa jana katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.

 

 

Utekwaji wa watu wa hivi karibuni, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni baadhi tu ya mambo yaliyotajwa katika waraka huo.

Serikali ya Tanzania kwa sasa imejibu kwa kusema kwa sasa haioni cha kujibu na kwamba inawatakia tu waumini kheri ya Pasaka.

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon