10 WAUAWA KWA AJILI YA WIZI WA MIFUGO KENYA
Wapatao watu 10 waliuawa na wengine kujeruhiwa Jumamosi katika kaunti ya Samburu nchini Kenya baada ya makabiliano kuzuka kati ya wafugaji na washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wezi wa mifugo.


Kamanda wa kaunti ya Samburu Alfred Agengo amesema kwamba kisa hicho kilitokea saa tatu asubuhi pale wafugaji walipofumaniwa na watu waliojihami kwa silaha katika eneo la Lupirio. Wenyeji wa eneo hilo wakisaidiwa na polisi walikabiliana na washambuliaji hao na kuua sita huku wafugaji wanne pia wakiuawa. Washambuliaji wanashukiwa kutoka kaunti jirani ya Pokot Magharibi na Baringo.


mzunguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu