HAZARD KUIKOSOA CHELSEA

March 23, 2018

 

 

 

 

Winga wa kimataifa wa Ubeligiji, Eden Hazard ameendelea kuikosoa klabu yake ya Chelsea na kocha wake Antone Conte. Hazard ambaye kwa sasa yupo kwenye timu ya taifa ya Ubeligiji amekaliliwa akikosoa bodi ya chelsea katika usajili uliopita.

-Hazard amedai hakufurahishwa na namna usajili wa dirisha la kiangazi lililopita. Chelsea walimtaka Romelu Lukaku ila deal lake halikukamilika na Chelsea wakaishia kumsajili Alvaro Morata.

-Hazard ambaye anacheza timu moja ya taifa na Romelu Rukaku amedai iwapo Chelsea wangemsajili mshambuliaji huyo angewasaidia sana kubeba makombe mbalimbali msimu huu akaenda mbali zaida akadai yeye anaelewana sana akicheza na Romelu Lukaku kwani kusingekuwa na shinda kwenye mfumo wa timu.

-Hii si mara ya kwanza kwa winga huyo kuikosoa Chelsea na Mbinu za Conte waziwazi aliwahi kukosoa mbinu za Conte kwa yeye kuchezeshwa kama false namba tisa kwenye mechi ya Uefa Champions League dhidi ya Barcelona pia alimkosoa Conte kwenye mchezo dhidi ya Man United kisa kumtoa mapema na Chelsea kupoteza mchezo huo.

-Imekuwa ni tabia ya wachezaji wa Ubeligiji kuteteana golikipa wa Chelsea, Thibaut Courtois naye alishawahi kukosoa mbinu za Conte mara kwa mara kwa kutolewa kwa mbeligiji mwenzake Hazard au kuchezeshwa kama mshambuliaji (False 9)

-Pia Hazard alishawahi kuwashauri wachezaji watatu kutoka Ubeligiji kuihama klabu hiyo alianza na Kelvin de Bruyne kipindi cha Mourinho akiwa anawekwa bechi sana alimshauri kuihama klabu hiyo, Mdogo wake Thorgan Hazard naye alimshauri kuondoka klabuni hapo ili aweze kupata timu ambayo itampa nafasi za kucheza mara mara na hivi karibuni alifanya hivyo tena kwa Michy Batchuayi kumshawishi kuihama klabu hiyo.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon