Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

MNANGAGWA AMPUUZA MUGABE

March 22, 2018

 

 

 

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa jana (Jumatano) alisema kwamba atapuuza pingamizi dhidi ya utawala wake na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, akisema kwamba Mugabe ambaye ana wa miaka 94 sasa amekuwa mkongwe na wa kusahausahau.

 

Mnangagwa alikuwa akijibu swali kutoka kwa mmoja wa wanahabari kwamba Mugabe huenda akakosa kumpigia kura katika uchaguzi ujao wa urais. “Bw Mugabe ni baba wetu mwanzilishi, tunamheshimu kwa hiyo. Lakini sasa ametimia miaka 94 na huenda akasahau kila mara alichosema,” alisema Mnangagwa. “Ukimuuliza mara nyingine atakuambia kwamba ananiunga mkono,” aliongeza Rais Mnangagwa.

 

Wiki jana Rais Mugabe aliambia waandishi wa habari wa kimataifa kwamba alilazimishwa kuondoka kwenye wadhifa wa urais kwa njia ya kijeshi. Kwenye mahojiano hayo ambayo yalikuwa ya kwanza kufanywa na Mugabe tangu kuondoka mamlakani, rais huyo wa zamani alidai kwamba utawala wa Rais Mnangagwa ni kinyume na sheria.

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload