Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

HALIMA MDEE NA MATIKO WASAKWE POPOTE WALIPO

March 22, 2018

 

 

 

Leo March 22, 2018 Wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mbunge wa Kawe Halima Mdee pamoja Esther Matiko ambaye ni Mbunge wa Tarime Mjini imeelezwa kuwa imetolewa amri na Polisi wakamatwe popote walipo.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amesema Mwenyekiti wa chama hicho Mbowe na viongozi wengine wameshindwa kufikishwa Mahakamani kwa kukosekana kwa kwa Wabunge hao wawili.'

 

Nanukuu kile alichoandika Lema “Mkti Mbowe na Viongozi wengine wameshindwa kufikishwa mahakamani kwa kuwa Halima Mdee/Easter Matiko (MB) hawakuweza kufika Polisi na amri imetolewa wakamatwe mahali popote walipo, John Mnyika na John Heche wamebaki polisi mpaka maelekezo mengine kutoka juu yatakapotolewa” -Lema

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload