RONALDO AKUTANA NA RUNGU LA KODI HISPANIA,
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo huenda akalipa serikali ya Hispania kodi ya euro milioni 14.7 ambayo alipatikana na hatia ya kukwepa kulipa iwapo hazina ya taifa itakubali kuondoa ombi la kufungwa kwake gerezani kwa kosa hilo, vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti.

Ronaldo na wawakilishi wake wanasemekana kujitolea kulipa gharama ya ushuru hiyo baada ya hazina ya taifa kupendekeza mchezaji mwingine wa Real Madrid Xabi Alonso kufungwa miaka nane gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi ya uero milioni 8. Hadi sasa Ronaldo na Xabi wamekanusha mashtaka hayo ya kukwepa kulipa kodi.

mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu