RAISI WA PALESTINA AWATUSI WAMAREKANI NA WAISRAELI

March 20, 2018

 

 

 

 

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas siku ya Jumatatu (jana) alimtukana Balozi wa Marekani na Israeli kama "walowezi" na "mwana wa mbwa".

Abbas aliyasema haya katika ufunguzi wa mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Uhuru wa Palestina (PLO) na kamati yake kuu ya Fatah iliyofanyika katika mji wa Ramallah.

"Utawala wa Marekani unadai kwamba makazi ya Israeli ni halali,na hivi ndivyo zaidi ya afisa mmoja wa Marekani alisema,ikiwa ni pamoja na balozi wao mjini Tel Aviv,David Friedman," Abbas alisema.

Abbas alisisitiza kwa hasira na kusema kuwa "mwana huyo wa mbwa"(Friedman) anasema wao (Israel) wanajenga katika nchi yao. Yeye ni walowezi na wanafamilia wake wote ni walowezi."

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon