MNANGAGWA AUWASHA MOTO ZIMBABWE

March 20, 2018

 

 

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza majina ya watu binafsi na mashirika ambayo hadi tarehe 16 Machi hayakuwa yamerudisha nchini humo mali na fedha za umma walizopora na kuficha katika nchi za kigeni.

Mnangagwa alisema kwamba kati ya jumla ya dola bilioni 1.4 (mali ya umma na pesa taslimu) zilizoporwa na kufichwa katika nchi za kigeni, dola milioni 591 zimerudishwa huku milioni 826.5 zikisalia. Rais huyo amesema kwamba bado kuna jumla ya dola milioni 464.2 pesa za umma ambazo zimefichwa kwenye benki za kigeni, dola milioni 237.4 ya thamani ya mauzo ya nje ambazo hazijafika kwenye mikono ya serikali na jumla ya dola milioni 124.8 zilizolipiwa bidhaa za kuagizwa kutoka nje lakini hazikufika nchini Zimbabwe

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon