KABURI LA HALAIKI LAGUNDULIKA IRAQ

March 20, 2018

 

 

 

 

Miili 39 ya raia wa India waliotoweka katika eneo la Mosul, nchini Iraq zaidi ya miaka mitatu iliyopita imepatikana ikiwa imezikwa kwenye kaburi la halaiki, waziri wa mambo ya kigeni wa India Sushma Swaraj ametangaza.

 

Maiti za waathiriwa hao waliouawa na kundi la kigaidi la ISIS zilitambuliwa kwa kutumia sampuli za DNA kutoka kwa jamaa zao. Miongoni mwa waathiriwa hao 39, 31 walikuwa wekazi wa jimbo la Punjab kaskazini mwa nchi, wanne kutoka jimbo la Himachal Pradesh huku waliosalia wakitoka majimbo ya Bihar na Bengal magharibi.

 

Maiti zote zilitambuliwa isipokuwa moja ambayo haingetambuliwa kwa kuwa wazazi wake hawako hai. Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa India V.K. Singh anatarajiwa kusafiri kuenda nchini Iraq ili kurejesha nchini maiti hizo 39 ambazo hatimaye zitakabidhiwa jamaa zao.

 

mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon