TRUMP ACHIMBWA MKWARA MZITO NA CHAMA CHAKE


Rais Donald Trump ameonywa na wanachama wa chama chake cha Republican kuacha kuingilia uchunguzi maalumu kuhusiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka wa 2016.


Hatua hii ya wanachama wa Republican inakuja baada ya rais Trump kumshambulia Mshauri Maalum, Robert Mueller, kuhusiana na uchunguzi wake dhidi ya Urusi kudaiwa kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Wanachama hao wamemtaka Rais Trump kutochukua hatua yoyote ikiwemo kumfuta kazi, Robert Mueller, ambaye ni mkuu wa zamani wa FBI na ambaye anaendelea kufanya uchunguzi huo.


"Akijaribu kufanya hivyo, itakuwa mwanzo wa miwsho wa madaraka yake, sababu sisi ni taifa la kufuata sheria," Senata Lindsey Graham alisema.

Katika ukurasa wake wa Twitter mwishoni mwa juma,Trump alirejea kutoa utetezi wake kuwa hakukuwa na uhusiano wowote kati ya timu yake ya kampeni na Urusi na kusema kuwa hiyo ni vita binafsi inayoshabikiwa na Democrats.Source:china shenhua news


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu