RAISI WA TFF ANENA JUU YA MAFANIKIO YAKERais wa TFF Wallace Karia anazungumzia mafanikio ya shirikisho tangu alipoingia Madarakani. TFF imekua ikiendesha michuano ya Azam Sports Federation Cup, Ligi ya Wanawake, Beach Soccer . Katika michuano ya Azam Sports Federation Cup, msimu huu timu zote zilipata huduma za usafiri na malazi kwa wakati kupelekea michuano hiyo kuwa na mafanikio mwaka huu. Ligi ya Wanawake imepata udhamini wa Serengeti Lite Premium Lager, jumla ya timu nane zinacheza ligi hiyo, kwa sasa ligi imesimama kutoa nafasi ya maandalizi ya timu Twiga Stars kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Zambia

Kwa mara ya kwanza ilifanyika michuano ya Beach Soccer, (Copa Dar es salaam) iliyoshirikisha nchi za Malawi, Uganda na Zanzibar. Hii ilitoa nafasi kwa makocha kupata nafasi ya kuona maendeleo ya wachezaji katika mpira wa soka la ufukweni


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu