MOROCCO YAJITOSA KOMBE LA DUNIA 2026Morocco imesema kwamba iko tayari kutumia dola bilioni 15.8 kwa ujenzi wa viwanja na miundombinu muhimu iwapo itapata fursa ya kuandaa kombe la dunia mwaka wa 2026.

Huku likimnukuu mwenyekiti wa kamati ya zabuni Moulay Hafid Elalamy, jarida la l'Economiste limeripoti kwamba sekta ya kibinafsi itachangia dola bilioni 3.2 ya bajeti hiyo.


Kando na kukarabati viwanja na kujenga vingine vipya, Morocco inapanga kujenga hospitali 21 na viwanja 131 vya kufanyia mazoezi. Wakipata zabuni ya kuandaa mashindano hayo, Morocco wanatarajia kupata nafasi 110,000 za kazi kila mwaka kutoka siku ya kushinda zabuni. Morocco inashindania zabuni hiyo dhidi ya Marekani, Mexico na Canada.


mzunguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu