ASKARI AGONGWA NA GARI DAR

Askari wa usalama barabarani anayejulikana kwa jina la Sajenti Peter amegongwa na gari leo asubuhi majira ya saa 5 wakati akitekeleza majukumu yake ya kusimamia usalama barabarani jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea katika makutano ya barabara ya Kajenge na Rose Garden eneo la Sayansi ilipokuwa akiongoza magari

Juma Husein ambaye ni mkazi wa Sinza amesema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina (EICHER) Daladala kushindwa kufunga breki baada ya kusimamishwa na trafiki na kisha kuligonga gari dogo aina ya Subaru ambalo lilikuwa limeruhusiwa kuondoka na kusababisha ajali iliyopelekea trafiki huyo kugongwa na gari jingine.

Ajali hiyo imetajwa kuhusisha magari matatu, majeruhi akiwemo trafiki huyo walikimbizwa hosptali kwa matibabu zaidi, aidha Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa trafiki huyo alivunjika mkono.

mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu