AFANDE SELE AJIUNGA RASMI NA CCM
Rapa mkongwe nchini Tanzania, Afande Sele ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi leo Machi 15, 2018 mkoani Morogoro mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Afande Sele amesema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na rushwa na kuwajali wanyonge.

Hata hivyo, Mfalme huyo wa Rhymes amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi wampokee kwa mikono miwili.


Afande Sele kabla ya kujiunga na CCM alishawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na Chama cha ACT Wazalendo ambapo mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Rais Magufuli leo Machi 15, 2018 amezindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro ambapo Afande Sele alitumia nafasi hiyo kujiunga na CCM.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu