IFAHAMU SAYARI YA MARS VIZURI KWA SASA.


Sayari ya Mars imekuwa ikiwashangaza, kuwasisimua na kuwavutia binadamu kwa miaka mingi.

Maelfu ya miaka iliyopita, binadamu walikuwa wakishangaa na kujiuliza nini kinapatikana katika sayari hiyo inayopatikana umbali wa kilomita milioni 54.6 kutoka kwa dunia (maili milioni 34).

Sana, kutokana na muonekano wake wa rangi nyekundu sawa na ya chuma iliyoshika kutu, binadamu waliihusisha na moto au damu.

Jina Mars linatokana na mungu wa vita wa Warumi.

Kutokana na ufanisi wa kisayansi, binadamu kwa sasa amefanikiwa kufahamu mengi kuhusu sayari hii.


Sayari hii ina mandhari ya kushangaza: utayapata maeneo sawa na ya nyika duniani, maeneo ya jangwa kutokana na upepo mkali, mashimo makubwa yanayotokana na volkano, milima ya volkano na maeneo ya ukubwa sawa na taifa la Luxembourg yaliyojaa milima (machungu) ya mchanga.

Haya yote yamefunikwa na vumbi ya rangi moja.


Ni eneo ambalo huwa hakuna mvua kamwe. Hakuwezekani kuwa na mvua kwani maji, iwapo yangekuwepo, hufusha na kuwa mvuke mara moja.


Katika sayari ya Mars, wakati sawa na wa kutua kwa jua duniani, anga hujaa rangi ya buluu. Dunia huonekana tu kama nukta tu miongoni mwa nyota angani.

Ni mandhari ya kupendeza sana hasa kwa wanaopenda utalii - ikizingatiwa kwamba binadamu hajatalii sana sayari hiyo, kuna uhakika kwamba iwapo utafanikiwa kufika huko, kila utatapoenda utakuwa binadamu wa kwanza kufika huko.


Utafikaje huko?

Kwa karne nyingi, imekuwa ndoto tu lakini inakaribia kutimia. Iwapo mambo yote yatakwenda sawa, mjasiriamali mmiliki wa Space X Elon Musk anapanga kutuma kundi la kwanza la watalii kwenye sayari hiyo kufikia 2022.

Lakini gharama yake itakushangaza pengine. Tiketi ni $10bn! Lakini iwapo huwezi kupata pesa nyingi kiasi hiki, usife moyo. Kuna njia nyingine ya kiteknolojia ambayo taasisi ya safari za anga za juu ya Marekani Nasa inatafakari - kutumia miwani ya kisasa na roboti. Roboti ndiyo itakuwa Mars, wewe uwe papa hapa duniani lakini itakuwa ikikupeperushia picha za uhalisia kutoka sayari hiyo.

Vivutio sayari ya Mars

Kivuti kikuu ni mlima wa Olympus Mons. Mlima huu una urefu wa maili 14 (kilomita 22), na ndio mlima wa volcano mrefu zaidi katika Mfumo wa Jua. Kwa kulinganisha tu, urefu wa mlima huu ni mara tatu urefu wa mlima mrefu zaidi duniani, Mlima Everest.

Sawa na ilivyo kwa milima mirefu ya volkano duniani, mlima huu kilele chake kimefunikwa na mawingu - lakini si ya maji, bali ni ya vumbi.

Haijabainika iwapo mlima huu bado hulipuka, lakini inakadiriwa kwamba wakati mmoja ulilipuka na kurusha matope na mawe makubwa ya moto angani.

Ukisafiri kusini magharibi kutoka kwa mlima huu, utapata Valles Marineris.


Hili ni bonde kubwa kwenye ikweta ya sayari ya Mars. Bonde hili linakadiriwa kuwa na umbali wa kilomita 4,000 ambao ni karibu na upana wa taifa la Marekani kutoka mashariki hadi magharibi.

Katika baadhi ya maeneo, bonde hili lina kina cha karibu kilomita saba (futi 23,000) - karibu mara nne kina cha bonde maarufu la Marekani ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Grand Canyon.

mingi Mars ina mito midogo ambayo inadhaniwa kuwa inatokana na michirizi ya maji yenye chumvi

Kufikia sasa, haijabainika bonde kubwa kiasi hiki liliundwa.

Bonde hili la Valles Marineris lina mchanga wenye marangi mbalimbali ya kupendeza ambao umejipanga kwa safu mbalimbali. Inadhaniwa kwamba huenda mchanga huu ulitokana na mashapo au machenga ambayo yalijikusanya chini ya ziwa au mto wa barafu, au kutokana na kujikusanya kwa majivu ya volcano.

Kinyume na bonde la Grand Canyon Marekani, ambalo liliundwa na mmomonyoko uliochota mchanga na kuyachonga mawe, kuna uwezekano kwamba bonde hili la Mars lilitokana na kutengana kwa maeneo mawili makubwa ya 'ardhi' ya Mars. Kila upande wa bonde hilo unaweza kuingia kwa ule mwingine, kana kwamba mtu anajaza mchezo wa fumbo.


Rangi ya anga

ati wa kutua kwa jua, anga huwa la rangi ya samawati

Ukafanikiwa kujipata kwenye bonde hili, na uwe unataka kuangalia kutua kwa jua, utashangaa kugundua kwamba anga lake halitakuwa ya rangi nyekundu - bali ya samawati. Hii inatokana na wepesi wa anga la sayari ya Mars, ambalo ni asilimia moja tu ya uzito wa anga la Dunia.

Anga la Dunia huwa rangi ya samawati mchana kutokana na miali ya jua kutawanywa na molekuli za hewa. Hili huwa halitendeki sana sayari ya Mars, hivyo mchana anga huwa la rangi ya manjano iliyokaribia hudhurungi. Lakini jua linapotua, ambapo miali yake huwa haina nguvu sana ndipo anga la Mars hugeuka na kuwa rangi ya buluu.

Sayari ya Mars pia ina jambo jingine la kushangaza. Katika maeneo mengi, chini ya vumbi lake jekundu, kuna mawe ya rangi ya samawati na kijani kutokana na madini kama vile chuma. Vumbi hilo linapobebwa na upepo au kutokana na kupita kwa sayari ndogo, huwa kunafichuliwa mandhari ya kupendeza ya mikolezo tofauti ya rangi ya samawati.


Hali ya hewa

Kiwango cha joto cha kadiri katika sayari ya Mars ni nyuzi joto takriban -56C (-69F). Hii ni sawa na hali ya baridi maeneo ya ndani kabisa ya Antarctica, anasema mtaalamu wa biolojia na anga za juu katika Chuo Kikuu cha Washington, David Catling.

Ndipo uweze kufurahia, itakubidi kukaa karibu na ikweta ya Mars, ambapo huko kiwango cha joto kinaweza kufikia takriban 35C (95F), na hakuna upepo sana. Kutokana na wepesi wa anga lake, upepo mkali huko utahisi kana kwamba ni upepo tu Ingawa huwa kuna unyevu na ukungu usiku katika sayari hiyo, mchana hali ni kavu sana.

Sababu ya chombo cha Ulaya kutoweka MarsMaji ya kale zaidi yagunduliwa Canada

Kutokana na hali kwamba sayari hiyo inapatikana karibu mara moja unusu mbali na jua ukilinganisha na Dunia, hakuna haja ya kuvalia miwani ya kukinga dhidi ya mwanga wa jua.

Huko, kuwasha moto pia ni ngoma kwani hakuna mimea na anga lake asilimia 96 ni kaboni daoksaidi - kemikali inayotumiwa kwenye mitambo mingi ya kuzima moto.

Tofauti na Dunia, ambapo mawingu na anga hufanya kazi kama blanketi na kuzuia joto kuondoka usiku, sayari ya Mars hakuna mawingu na anga lake ni jepesi sana. Matokeo yake ni kwamba, sawa na inavyofanyika jangwani, usiku huwa kuna baridi kali sana. Baridi hii inaweza kufikia nyuzi -73C (-99F) usiku karibu na ikweta kwenye sayari hiyo.


Viumbe wote walio hai duniani huwa wana maji ndani yake. Hivyo, wataalam wamekuwa wakiamini kwamba iwapo kuna viumbe Mars, lazima wawe kwenye maeneo yaliyo na maji.

Kwa miongo mingi, wanasayansi walitafuta ishara za kuwepo maji Mars bila mafanikio.

Lakini mwaka 2011, walifanya ugunduzi huo. Waligundua michirizi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kwa milima na mabonde ya Mars. Inadhaniwa kwamba huenda mito, yenye maji yenye chumvi labda huchipuza kutoka chini ya 'ardhi' kwenye hazina kubwa ya maji.


Kutokana na kiwango cha chini ya nguvu mvuto, uzani wa vitu huwa tofauti sayari ya Mars. Binadamu wa kilo 100 hivi, uzani wake Mars unaweza kuwa karibu na kilo 38 hivi.

Ukafanikiwa kutua kwenye Mars, utakuwa ukiitazama Dunia na kuiona kama tone au kituo angani. Dunia utaiona ikiwa sawa na tunavyoiona sayari ya Zuhura mapema asubuhi, au jioni angani, anasema Catling.MZUNGUKO.COMTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu