CHELSEA YAKUBALI MATESO TOKA KWA BARCELONA UEFA ,ASRENAL WENGER AJITETEA,

Katika Premier League nchini England , kocha Arsene Wenger anakiri kwamba Arsenal inasumbuka kuwavutia tena mashabiki ambao wamekasirishwa baada ya maelfu kubakia nyumbani licha ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Watford jana Jumapili.Arsenal ililaumu kwamba kuanguka kwa theluji ndiko kulisbabisha mashabiki kuwa wachache uwanjani katika kipigo chake cha hivi karibuni dhidi ya Manchester City , lakini kutokujitokeza tena kwa mashabiki wengi dhidi ya Watford kunaweza tu kuwekwa pamoja kwa mchanganyiko wa hasira na kukata tamaa baada ya msimu mwingine mbaya.


Champions League inarejea tena uwanjani wiki hii , ambapo Barcelona na Manchester United zina michezo ya nyumbani kesho na Jumatano dhidi ya Chelsea na Sevilla ya Uhispania. Timu hizo zinaingia katika mapambano hayo ya mwisho ya timu 16 zilizobakia katika Champions League zikitaraji sare katika mkondo wa kwanza ugenini zinaweza kuwaingiza katika robo fainali ya michuano hiyo.

United inaikaribisha Sevilla kesho Jumanne huku matokeo ya mwanzo yakiwa 0-0, wakati Barca inaikaribisha Chelsea iliyotoka nayo sare ya bao 1-1 uwanjani Stamford Bridge.Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema wachezaji wake wajitayarishe kuteseka dhidi ya barcelona siku ya Jumatano ,iwapo watataka fursa ya kuendelea katika robo fainali ya Champions League.

Bayern Munich inaelekea Uturuki siku ya Jumatano kupambana na Besiktas huku ikiwa na hakika ya kuendelea katika duru ya robo fainali baada ya kupata ushindi mnono uwanjani Allianz Arena wa mabao 5-0 , wakati Roma ikiwa nyumbani inapimana nguvu na Shakhtar Donetsk ya Ukraine huku matokeo ya mchezo wa kwanza yakiwa mabao 2-1 kwa upande wa klabu hiyo ya Ukraine.


CHANZO:DW


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu