Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Picha ya kuokolewa kwa chui yashinda tuzo

November 22, 2017

 

Mnamo Julai 19, 2012, Anand Bora alipokea simu isiyo ya kawaida saa mbili asubuhi na kufahamishwa kwamba chuo alikuwa amekwama kwenye kisima katika kijiji kimoja jimbo la Maharashtra, magharibi mwa India.

Bw Bora alikimbia kwenye kijiji hicho cha Bubali na kupiga picha operesheni ya zaidi ya saa tatu unusu ya walinzi wa msitu na wanakijiji wakijaribu kumuokoa chui asife maji kisimani.

Ni mwalimu lakini mpiga picha na alipiga picha za kipekee siku hiyo.

Katika moja ya picha hizo, chui huyo kuwa anaonekana akitazama juu kuwaangalia wale waliokuwa wanamuokoa.

Picha hizo ilishinda tuzo ya upigaji picha wa wanyamapori nchini India wiki iliyopita.

Ushindi wake umeibua maswali kuhusu yaliyojiri wakati wa uokoaji huo.

Picha hiyo ya miaka mitano iliyopita ni ya kipekee kwani mara nyingi wanyamapori hushambuliwa na kuuawa na wakazi.

"Chui huyo alipotazama juu, anaonekana kuhisi kwamba hatungemuumiza, kwamba tulikuwa tunajaribu kumuokoa," Bw Bora ameambia BBC.

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload