ELIMU JUU YA TETENASI ( TETANUS)


Tetenasi ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria wanaoitwa ( Clostridium tetani). Wadudu hawa wanapatikana katika mazingira yanayotuzunguka mfano; ardhini,, misumari au vitu vyenye ncha, vinyesi vya baadhi ya wanyama nk. Bacteria wa tetenasi wanaweza kuishi katika mazingira kwa miaka mingi. Pia wanapenda vidonda, ndio maana wanaingia mwilini kupitia vidonda au mikwaruzo. Dalili za Tetenasi zinatokea siku 4-14 baada ya kupata jeraha. Tetenasi imegawanyika sehemu mbili.

 1. Tetenasi inayotokea kwa watu wazima (adult)

 2. Tetenasi ya watoto (neonates)

Nani yupo hatarini kupata tetenasi? Kwa watu wazima (Adults)

 1. Ikiwa umeumia na kupata jeraha au kidonda sehemu ya mwili wako uko katika hatari ya kupata ugonjwa huu hatari wa tetenasi.

 2. Ikiwa umetobolewa na msumari una zaidi ya 32% kupata tetenasi.

 3. Ikiwa umeungua, au watu wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya, au watu wanaojiwekea tattoo, watu wenye magonjwa ya meno, wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu

 4. Kisukari ni moja ya hali inayoweza kukusababishia tetenasi.

 5. Pia upasuaji (surgery) isiyo salama, mfano matumizi ya vyombo visivyo salama(unsterilized)

Kwa watoto.

 • Kama mama mjamzito hatapata chanjo ya tetenasi , au kujifungulia nyumbani, yupo kwenye hatari ya kumsababishia mtoto mchanga kupata tetenasi.

Dalili za Tetenasi.

 1. Kukakamaa kwa misuli, mdomo kushindwa kufunguka(lock-jaw)

 2. Kutokwa na jasho jingi, homa kali

 3. Kushindwa kumeza kwasababu ya kukakamaa kwa misuli.

 4. Kutokwa na udenda(drooling).

 5. Kupata matatizo ya kupumua.

Kinga.

 • Tafadhali nenda hospitalini au kituo cha afya mara baada ya kupata jeraha lolote ili kupata chanjo ya tetenasi.

 • Kwa wafanyakazi wa afya, ni muhimu kupata chanjo ya tetenasi kwasababu ya mazingira hatarishi ya kazi.

 • Kwa mama mjamzito tafadhali hakikisha unapata chanjo zote za tetenasi ili kujikinga na pia kumkinga mtoto. Pia unapoona dalili za uchungu hakikisha unawahi ukajifungulie kituo cha afya mapema.

 • Epuka majeraha yasiyokua ya lazima, vaa viatu, weka vitu vyenye ncha kali mbali na watoto.

 • Mpeleke mtoto atahiriwe hospitalini na sio mtaani, kwasababu ya hatari kubwa iliyopo ya kupata tetenasi.


Tufuate kupitia:
 • YouTube Social Icon
 • Twitter Social Icon
 • Black Instagram Icon
 • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu