WATU WENYE SIFA HII NDIYO WANAOFANIKIWA

Linapokuja swala la mafanikio zipo sifa na mambo mengi ambayo yanakuwa yanatajwa katika kumfikisha mtu ili aweze kufanikiwa. Mambo au sifa hizo huwa ni za msingi sana kwa kila mtu ili kufikia mafanikio. Hata hivyo pamoja na sifa hizo, ipo sifa moja muhimu sana ambayo kwa mtafuta mafanikio kama unayo ni lazima utafanikiwa. Sifa hii muhimu ya kimafanikio ambayo nataka kuiongelea hapa ni uvumilivu wako katika kuelekea mafanikio. Unaweza ukawa unajituma kweli, una nidhamu binafsi na unafanya juhudi za kuwekeza kila wakati, lakini ukikosa uvumilivu hasa pale unapokutana na changamoto au pale unaposubiri mafanikio yako makubwa huwezi kufanikiwa. Uvumilivu ni kitu cha muhimu sana kama umeamua kuishi maisha ya ndoto zako. Inabidi uvumilie hali ngumu unazokutana nazo, inabidi uvumilie kuishi wakati mwingine chini ya kipato ili kutimiza malengo ya ndoto zako. Kuna kitu najua unataka kujiuliza nitavumilia mpaka lini, mbona maisha yangu naona kama magumu, hayaeleweki na hii biashara italeta mafanikio lini? Ndio, najua yote hayo unapitia, hakuna namna zaidi ya wewe kukomaa na kukubali kuvumilia. Sikiliza, kiuhalisia mara nyingi inachukua miaka 3 hadi 5, ili kuweza kupata mafanikio ya uhakika kwa kile ambacho umekianzisha leo. Huo sio muda mrefu sana kama unavyofikiri. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na subira na kuweka juhudi sana kila siku. Hebu jiulize kuna yale mambo ambayo uliyaanza miaka mitatu iliyopita, yanaonekana kama yalianza jana tu. Kama hiyo iko hivyo hata maisha yako unaweza kuyabadili. Kwa nini usikubali kuvumulia ili kutengeneza ndoto zako za kimafanikio. Hata kila unayemwona amefanikiwa, au kila unayemwona yupo ngazi fulani ya kimafanikio kuna mengi ambayo amepitia na kuvumulia hadi akavuna hicho alichokivuna. Kama hutaki kuwa na uvumilivu, utajiweka pembeni kwenye njia ya mafanikio wewe mwenyewe. Huna haja ya kujiona unachelewa, hebu jipe muda wa kubadili ndoto zako. Uwe na uhakika hilo litafanikiwa na utajenga maisha ya mafanikio unayoyataka wewe. Watu wenye sifa ya kuvumilia magumu mengi na kuweka juhudi hao ndio wanaofanikiwa. Hakuna hata siku moja mtu ambaye akipata hasara kidogo anaacha biashara eti akafanikiwa, mtu hayupo. Uvumilvu wako ni muhimu sana katika safari ya mafanikio uliyoichagua. Ukiona huna uvumilivu wa kutosha, SAHAU MAFANIKIO.

mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu