Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Deontay Wilder: Anthony Joshua haniwezi hata kidogo

November 9, 2017

 

 

 

 

Bingwa wa ndondi katika uzani wa WBC Deontay Wilder anasema kuwa atampiga Anthony Joshua nyumbani kwake Uingereza.

Wilder mwenye umri wa miaka 32 alitetea taji lake dhidi ya Bermaine Stiverne siku ya Jumamosi , wiki moja baada ya Joshua kuhifadhi taji lake la ukanda wa WBA na IBF dhidi ya Carlos Takam mjini Cardiff.

''Viwanja vilivyojaa watu vinaonekana vizuri lakini Mecca ya ndondi ipo Marekani'', Wilder aliambia BBC Sport.

''Lakini kama unataka kusalia nyumbani kama msichana mdogo mfalme huyu hajali kuja na kumwangusha bingwa''.

 

Katika mahojiano na BBC Radio 5, Wilder alimshutumu promota Eddie Hearn kwa kuwadanganya mashabiki kwamba Joshua ndio bondia bora katika uzani mzito duniani.

''Iwapo Joshua ndio bora, na bingwa , Waingereza wanafaa kumwambia ajitokeze na apigane ndio mujue kwamba yeye ndio bora''.

''Moyo wangu unaniambia kwamba mimi ndio bora na kama sio bora basi ningependa aliye bora aje anionyeshe''

 

Mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload