Wana wa ufalme wakamatwa Saudi Arabia

November 5, 2017

 

Mawaziri 11 miongoni mwao wakikwa wana wa ufalme wameachichwa kazi na hata kuzuiliwa katika Mabadiliko makubwa yaliyotangazwa kwenye serikali ya Saudia.

Wengine wanaozuiliwa ni mawaziri wa zamani ambao wamehusishwa na kashfa za rushwa.

Katika hatua hiyo ambayo si ya kawaida inaelekea mwana mrithi wa mfalme Mohammed Bin Salman ambaye ndiye anaesimamia kitengo cha kupambana na ufisadi, anapania kujitenga na kuwadhibiti wapinzani wake wenye mamlaka makubwa nchini humo.

  • Qatar kudai fidia kutoka nchi zilizoitenga

  • Mfalme wa Saudia, ziarani Urusi

Miongoni mwa wanazuiliwa ni wana wa wafalme mmojawao ni mtoto wa marehemu mfalme Abdullah Prince Miteb aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kikosi cha kiusalama National guard ambapo sasa amepokonywa wadhfa huo.

 

Mwengine ni billionaire Prince Al-Waleed bin Talal.

Inaripotiwa kwamba hisa katika kampuni aliyoekeza huko uingereza iitwayo Kingdom Holding, zimeporomoka kutokana na hisia hizo.

  • Ayatollah Khamenei aishtumu Saudia inavyosimamia Hajj

  • Mataifa ya Kiarabu yajitenga na Qatar

Mwandishi wa BBC anaefuatilia kwa karibu swala hilo anasema mabadiliko hayo bila shaka yatawabugudhi wale wanaopendelea mambo yabaki yalivyo Saudia ambako wenye mamlaka ya juu ya kiukoo na kikabila hawapendelei hatua kama hizo za kubadili mambo gafla.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon